Friday, May 27, 2016

Kilimo cha matikiti maji



Ili kulima matikiti maji, inakubidi uwe na sehemu ya kutosha, yenye jua la kutosha, maji mengi na ardhi yenye rutuba ya kutosha, matikiti maji hukua haraka kama mimea mimgine ya jamii yake itambaayo mfano Matango, maboga na maskwash.
Kwa mtu ambaye anaanza kilimo yatampa tabu kidogo tofauti na Yule ambaye ana ujuzi kidogo na mambo ya kilimo kwa sababu yanahitaji umakini kiasi.

HALI YA HEWA
Mimea hii haihimili hali ya joto kali sana, mvua nyingi na udongo unaotuamisha maji, magonjwa ya fangasi na wadudu waharibifu, inastawi vizuri kwenye kuanda wa pwani na miinuko kidogo kama DSM,Tanga, Morogoro, Mtwara, lindi na Pwani ambapo kuna jua la kutosha. Muda mzuri wa kupanda ni kipindi cha kipupwe mwezi wa machi mpaka wa septemba .

UPANDAJI
Panda kwa kutumia Mbegu zinazouzwa madukani, ukitumia Mbegu kutoka kwenye tikiti ulilonunua linaweza likawa ni hybrid na matokeo yake matikiti yatakayozaliwa hayatakuwa bora kwa sababu yatakuwa ni kizazi cha pili (F2)
Panda Mbegu yako moja kwa moja kwenye shamba, usinunue miche au kupanda Mbegu kwenyemifuko ya plastiki halafu ndi uhamishie shambani, panda Mbegu mbili sentimeta 2 chini ya udongo kwa umbali wa sentimeta 30 kutoka shina hadi shina na mita 2 - 3 kutoka mstari hadi mstari, baada ya siku chache Mbegu zitaanza kuota, baada ya kama wiki 2 katika Mbegu mbili ulizopanda kata moja na uache ule mche wenye afya zaidi, angalizo using’oe mche bali ukate ili kuzuia kusumbua mizizi ya mche uliobaki.
Unaweza kupandishia udongo kwenye mashina na hii itasaidia kupunguza maji yasituame kwenye mimea yako, pia unaweza kuweka samadi badala ya kupandishia udongo ukiwa na nia ileile ya kuzuia maji yasituame na kuongeza rutuba.
Kama una sehemu ndogo ya shamba unaweza kuyawekea matikiti waya wa kutambalia, ila inabidi uwe imara kwa sababu ya kuhimili uzito wa matunda yenye, na wakati wa kuanza kutambaa kwenye waya ni lazima uifundishe mimea kwa kuielekezea kwenye waya na kufungia.

UANGALIZI
Miche ikiwa imetambaa kiasi unaweza kuweka matandazo kwenye udongo ili kuzuia upotevu wa unyevu, unaweza kuweka samadi au mbolea za viwandani, mimea ikiwa midogo tumia zaidi mbolea zenye nitrojen na utumie zaidi mbolea za potasiam mara baada ya maua kutokeza hadi matunda kukomaa, matawi yakifikia urefu wa mita 2 kata mbele ilikuruhusu kutoa matawi na hivyo kupata maua mengi zaidi hatimaye mavuno zaidi

MAUA NA MATUNDA
Matikiti hutoa maua dume na jike kwenye tawi moja, maua dume ambayo ni madogo zadi hutoka kwanza yakifuatiwa na maua jike ambayo ni makubwa zaidi, usipoona maua dume na jike kuna tatizo mfano maji kidogo yalimwagiliwa, upungufu wa viritubisho kwenye udongo, hali ya hewa ni joto/baridi sana n.k
Uchavushaji kwenye matikiti hufanyika na wadudu, kama huwaoni wakifanya kazi yao unaweza kufanya mwenyewe, muda mzuri ni wa asubuhi, unakata maua dume kwa kisu na kufanya uchavushaji kwenye maua jike, maua jike ya mwanzo kwenye tawi ndiyo yenye ukuaji bora zaidi, unaweza kukata tawi lisiendelee kukua baada ya matunda kutokeza hii husababisha kuwa na matunda makubwa zaidi.

UVUNAJI MATIKITI
Ili kujua matikiti yamekomaa inahitaji ujuzi kidogo, upande wa chini wa tunda huanza kuwa na rangi ya njano, pia kikonyo juu ya tunda hukauka kabisa na kuwa kijivu, ila njia nzuri ni kuyapiga kwa kiganja na kusikiliza mlio wake kama tunavyofanya kwenye mafenesi, hii nayo ni shule nyingine. Tumia kisu wakati wa kuvuna matikiti, yabebwe na kuhifadhiwa vizuri kwenye makasha tayari kuuzwa au kwa matumizi binafsi

MAGONJWA NA WADUDU
Wadudu wa matikiti wako wanaoshambulia majani na maua, na wengine hushambulia matunda , pia kuna magonjwa ya fangasi ambayo hushambulia mimea, ili kujua dawa za magonjwa ni vizuri kuchukua sampuli na kwenda nayo kwenye duka la dawa na pembejeo za kilimo ili kjupata dawa sahii, dawa aina ya KARATE itasaidia kuua wadudu wa majani, maua na matunda na FUNGICIDE itasaidia kwa mashambulizi ya fangasi.




This entry was posted in

KILIMO BORA CHA NYANYA



Utangulizi
Nyanya ni zao la chakula na biashara. Kilimo cha zao hili hufanyika majira yote
(masika na kiangazi), na faida hupatikana haraka na ni ya kuridhisha ikilinganishwa
na mazao mengine. Pamoja na umuhimu wa zao hili, wadudu waharibifu na
magonjwa huathiri uzalishaji na ubora wa matunda. Ili mkulima aweze kupata faida
na kuongeza pato la kaya yake ni vema kuzingatia udhibiti wa magonjwa na wadudu
wa zao hili. Kipeperushi hiki kinatoa maelezo ya udhibiti wa magonjwa na wadudu
muhimu ya zao la Nyanya.
MAGONJWA YA NYANYA
Bakajani chelewa (Late blight)
Ugonjwa huu huenenzwa na vimelea vya fangasi. Husababishwa na hali ya hewa hasa
ya unyevunyevu, na huenezwa na upepo. Majani, shina, matunda hushambuliwa.
Majani huwa na ukungu mweupe na kijivu, na baadaye hukauka. Matunda huwa na
mabaka ya kikahawia na baadaye kuoza. Mashina pia huwa na mabaka ya kikahawia.
Udhibiti
· Nyunyiza dawa ya kuzuia ukungu hasa wakati wa masika, Dawa
zinazopendekezwa ni Ridomil, Dithane 45, Bravo, Funguran, milraz.
· Fanya mzunguko wa mazao. Usipande nyanya sehemu moja kila msimu au
palipolimwa mazao jamii ya nyanya km viazi mviringo, bilinganya, aina zote
za pilipili na nyanya chungu.
· Tumia mbegu safi
· Panda aina za nyanya zinazovumilia ugomjwa
Bakajani tangulia (Early blight)
Huenezwa na vimelea vya fangasi. Husababishwa na kuenezwa na hali ya hewa
pamoja na mbegu zenye ugonjwa. Mabaka ya kahawia yenye mistari ya mviringo
huonekana kwenye majani na shina. Baka jeusi hutokea sehemu ya tunda
inayoshikana na kikonyo.
Udhibiti
· Nyunyiza dawa ya Kocide, Funguran
· Teketeza mabaka ya mazao baada ya kuvuna
· Tumia mbegu safi na bora
Mnyauko fusari (Fusarium wilt)
Huenezwa na mbegu zenye ugonjwa. Husambazwa na vimelea vya fungasi
vinavyoishi kwenye udongo.
Ugonjwa hujitokeza zaidi wakati wa kiangazi. Vimelea hushambulia sehemu au
mirija ya mmea ya kupitishia maji na chakula. Mmea hukosa maji na chakula na
hatimaye hunyauka. Shina la mmea likipasuliwa ndani huonekana rangi ya kikahawia.
Udhibiti
· Tumia mbegu safi na bora
· Tumia mzunguko wa mazao. Nyanya zisizungushwe na mazao jamii yake
· Teketeza masalia ya mimea
· Choma kitalu cha nyanya kabla ya kusia mbegu
Mnyauko bacteria (Bacterial wilt)
Ugonjwa husababishwa na vimelea vya bacteria vinavyoishi kwenye udongo.
Huenezwa na kusambazwa na mbegu na udongo wenye vimelea. Mirija ya mimea ya
kupitishia maji na chakula hushambulia na mimea hunyauka ghafla. Mmea hukauka
na kufa.
Udhibiti
· Panda mbegu safi
· Panda nyanya sehemu ambayo haijawahi kupandwa viazi mviringo,
bilinganya au nyanya chungu
· Tumia mzunguko wa mazao
· Hakikisha mfereji wa maji ya kumwagilia hayapiti kwenye shamba lenye
historia ya ugonjwa huu.
· Choma kitalu cha nyanya kabla ya kusia mbegu
Mnyauko vetisili (Verticillum wilt)
Hakuna dawa inayozuia au kutibu ugonjwa huu kwa sasa. Ugonjwa husababishwa na
ukungu (fangasi) kwenye udongo. Ukungu huu huishi kwenye udongo kwa muda
mrefu bila kudhurika. Ugonjwa huongezeka ikiwa mizimizi ya nyanya
imeshambuliwa na minyo fundo; au kukiwepo na hali ya ubaridi au ukame. Ugonjwa
husababisha hasara kubwa. Ugonjwa hushambulia sehemu ya ndani ya shina na
kusababisha sehemu hiyo kuwa na rangi ya kijivu. Majani hugeuka njano na mimea
kunyauka na kufa.
Udhibiti
· Tumia mzunguko wa mazao usiopungua miaka mine
· Ondoa mabaki ya nyanya shambani
· Tumia mbegu bora na safi
Bakadoa (Bacterial spot)
Ugonjwa huu huenezwa na vimelea vya bacteria vinavyoishi kwenye mbegu, pia
kwenye hewa. Huenezwa kwa kasi sana wakati wa masika. Madoa ya rangi kahawia
huonekana kwenye majani na matunda.
Udhibiti
· Panda mbegu bora na safi
· Tumia mzunguko wa mazao
· Teketeza masalia ya mazao
· Nyunyizia dawa ya funguran, Kocide101, Cobox, Bravo
Makovu bakteria (Bacterial canker)
Ugonjwa huenezwa na vimelea vya bacteria vinavyoishi kwenye mbegu na hewani.
Hutokea zaidi wakati wa masika. Majani hukauka nchani na makovu yaliyodidimia
hutokea kwenye shina. Matunda huwa na makovu yenye rangi ya kahawia sehemu ya
katikati.
Udhibiti
· Tumia mbegu bora na safi
· Teketeza masalia ya mazao
· Tumia mzunguko wa mazao
2
Rasta (Yellow leaf curl)
Ugonjwa huu husababishwa na virusi na huenezwa na nzi wadogo weupe. Hutokea
zaidi wakati wa kiangazi. Mimea hudumaa na majani yaliyoshambuliwa huwa na
rangi ya manjano na pengine rangi ya zambarau. Nyanya hupasuka.
Udhibiti
· Nyunyiza dawa za sumu za kuua wadudu (Selecron, Dursburn, Actelic)
· Ng’oa mimea yenye ugonjwa
· Tumia mzunguko wa mazao
· Weka shamba katika hali ya usafi
Batobato (Tomato mosaic virus)
Ugonjwa husababishwa na virusi na hueezwa na mbegu na kugusana. Majani huwa na
mchanganyiko wa rangi hasa kijani kibichi na kijani kilichofifia (majano). Majani
hujikunja na manjani machanga huwa na maumbile yasiyo kawaida. Ukifikisha jani
huwa linavinjikavunjika.
Udhibiti
· Tumia mbegu bora na safi
· Ng’oa mimea iliyoshambuliwa
· Teketeza masalia ya mazao
· Weka shamba katika hali ya usafi
WADUDU WAHARIBIFU
Viwavi Matunda (Fruit worm)
Viwavi hawa hutokana na wadudu nondo. Viwavi hutoboa matunda na kuacha
matundu na hatimaye matunda huoza. Hupunguza ubora wa matunda.
Udhibiti
Nyunyizia dawa ya kuua wadudu. Dawa hizo ni pamoja na Actelic 50EC, Selectron,
Dursbaan, Maji ya majani ya mwarobaini au utupa pia huua wadudu.
Utitiri wekundu (Red Spider mites)
Hawa ni wadudu wekundu, wadogo sana wanaoweka utando chini ya majani, hasa
wakati wa kiangazi. Wadudu hawa hufyonza utomvu kwenye majani na kusababisha
majani kukauka.
Udhibiti
· Nyunyizia dawa za sumu. Dawa hizo ni pamoja na Actellic, Selecron,
Dursbarn na Thionex
· Mwagilia maji mara kwa mara
· Weka shamba katika hali ya usafi
Inzi weupe (White flies)
Hawa ni Inzi weupe wadogo sana. Hujitokeza sana wakati wa kiangazi. Hueneza
ugonjwa wa virusi ujulikanao kama Rasta.
3
Udhibiti
Nyunyizia dawa za sumu za kuulia wadudu kama Selecron, Actellic, Dursban na
thionex. Pia maji ya majani ya mwarobaini na utupa.
Vidukari au Wadudu mafuta (Aphids)
Ni wadudu wenye rangi nyeusi au kuijani au kahawia. Hukaa chini ya majani na
kufyonza utomvu kwenye majani machanga. Hudumaza mmea na kushindwa kuzaa
matunda
Udhibiti
Nyunyizia dawa za sumu za kuulia wadudu kama Rogor, Actellic, Selecron, Dursban
maji ya majani ya mwarobaini na utupa, maji ya pilipili.
Minyoo (Nematodes)
Ni minyoo midogomidogo ambayo hushambulia mizizi na kuweka vifundo. Mizizi
hushindwa kuchukua maji na chakula kwenye udongo. Mimea hudumaa na
kushindwa kuzaa
Udhibiti
· Tumia mzunguko wa mazao
· Choma udongo wa kitalu kabla ya kusia mbegu kwa kutumia karatasi la
plastiki jeusi na nishati ya jua
· Choma masalia ya mazao
Sota (Cutworms)
Hushambulia miche ya nyanya hasa baada ya kupandikizwa shambani. Wakati wa
mchana hujificha kwenye udongo na usiku hujitokeza na kukata miche kwenye shina
usawa wa udongo.
Udhibiti
· Nyunyiza dawa za kuua wadudu kwenye shina usawa wa udongo
· Hakikisha miche inapata maji ya kutosha.
This entry was posted in

Rekodi ya ubingwa Yanga

Kikosi-cha-yanga-machi-bongosoka

Yanga imefanikiwa kuweka rekodi ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara kwa mara ya 26 mwaka huu, ubingwa ambao tangu kuanzishwa kwa Ligi Kuu Tanzania Bara hakuna timu yoyote iliyofikia idadi hiyo.
Simba ya Dar es Salaam yenye upinzani na Yanga inashika nafasi ya pili ikiwa imetwaa mara 18. Pia  Mrundi Amissi Tambwe  amevunja rekodi kwa  kufunga mabao 21 hadi sasa katika ligi hiyo na kuvunja rekodi ya Abdallah Juma aliyefunga mabao hayo 20 ndani ya kipindi cha miaka 10 iliyopita.
Rekodi ya kufunga mabao mengi inashikiliwa na Mohammed Hussein ‘Mmachinga’ aliyefunga mabao 24 katika ligi hiyo mwaka 1994. Tambwe pia ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa kigeni nchini kufunga zaidi ya mabao 20 katika ligi Tanzania.

Tambwe pia ameweka rekodi mpya ya kuwa mchezaji mwenye mabao mengi zaidi Ligi Kuu Tanzania Bara ndani ya kipindi cha misimu mitatu tu baada ya kufunga mabao 54.

Jose Mourinho atua rasmi Manchester United


 Manchester United leo imemtangaza Jose Mourinho kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo baada ya Mreno huyo kusaini mkataba wa miaka mitatu leo.

Jose Mourinho ametangazwa na klabu ya Man United  lakini atajiunga na kuanza kufanya kazi rasmi msimu wa mwaka 2016/2017 hii ina maana tutaanza kumuona Mourinho akiiongoza Man United  kama kocha mkuu wakati wa mechi za maandalizi ya mechi za msimu zitakazo fanyika nchini China.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Jose Mourinho alifukuzwa kazi na Chelsea December 2015,  kocha huyo mwenye asili ya Ureno toka mwaka 2003 hadi sasa akiwa kama kocha amefanikiwa kushinda jumla ya Makombe 23 katika nchi 4 tofauti.

Saturday, May 21, 2016

SMS TAMU ZA KIMAHABA

Image result for love sms

Utamu wako ni zaidi ya asali, ni wa asili usiohitaji kuongezewa ladha ya sukari, nitaumiss endapo kama ukiwa mbali "NIACHE NIKUPENDE SWEET"

Furaha ni kawaida yangu, kununa si busara kwangu, kuishi nawewe vizuri ni sehemu ya Maisha yangu, kukusalimia ni hulka ya Moyo wangu, Uhali gani mpenzi?

Nakupenda sana D tafadhari usinikasirikie, nimekukumbuka nahitaji kukuona unipoze moyo wangu,njooo mwandani wangu nakusubiri daktari wangu.



Mpenzi wangu kukutana nawe ilikuwa ni bahati, kukuchagua kuwa rafiki yangu ilikuwa ni maamuzi yangu, lakini kuanguka kwenye penzi lako haikuwa hiyari yangu. Umeniteka moyo na akili yangu pia.

Usiku wa leo uwe ni wenye faraja kwako, utawaliwe na usingizi wa mahaba kwenye kope zako,
naomba ujenge taswira yangu katika mawazo yako, Usisahau kuniota sweet wangu. USIKU MWEMA.

Si vibaya mimi kukusifia kwani wewe ni wangu, nivingi umejaaliwa, vinavyouvutia moyo wangu, ama hakika uzuri wako umedhibiti matamanio yangu "SINTOMPENDA MWINGINE ZAIDI YAKO"



Thamani ya Mapenzi yako nikubwa kwangu, haifanani nachochote kwenye huu ulimwengu, sina budi kumshukuru mungu, kwa kunijaalia mpenzi mwema unaejali hisia zangu, USICHOKE KUNIPENDA MPENZI.

Wewe ni wapekee ninaekupenda, sifikirii kukusaliti na wala sina wazo la kukutenda, nakuomba tuendelee kupendana siku zote sweety wangu.

Dhamira kuu ya Moyo wangu ni Mapenzi, kukupenda kwa dhati bila kipingamizi, kuishi nawewe kihalali kwa kudra za wazazi, Nipende nikupende Tudumishe Mapenzi.



 *°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*Uchungu wa kifo hauna tofauti na maumivu nitakayoyapata ukiniachana, mpenzi usiniache nami siko tayari kukuacha.
       *°·.¸¸.°  ♥  °·.¸¸.°*

Friday, May 20, 2016

NJIA NNE ZA UHAKIKA ZA KUPATA MTAJI WA KUANZISHA BIASHARA


Moja ya changamoto ambazo watu wengi wanaotutafuta huwa ni wanawezaje kupata mtaji wa kuanza biashara. Hiki kimekuwa kikwazo kwa watu wengi kuingia kwenye biashara. Hata wale ambao tayari wapo kwenye biashara, wamekuwa wakitamani kukuza biashara zao ila wanashindwa kutokana na kukosa fedha za kuingiza kwenye biashara.

Kama wewe unapenda biashara, na umepanga kuingia au umeshaingia lakini hujaweza kukuza mtaji wako, hapa tutakupa njia mbalimbali za kupata mkopo kwa ajili ya biashara yako.



  1. Fedha zako binafsi.
Njia nzuri sana kwako kupata mtaji wa biashara ni kwa kuanza kuweka akiba ya fedha zako mwenyewe. Kama umeajiriwa anza utaratibu maalumu wa kuweka kiasi cha fedha pembeni ambacho hutakigusa hata iweje. Baadae unaweza kukitumia kwenye kuanza biashara. Kama hujaajiriwa unaweza kutafuta shughuli yoyote ukafanya na hii ikakuingizia kipato ambacho baadae utaweza kuanzia biashara.
  1. Michango kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki.
Kama unaweza kukaa chini na ndugu zako na ukawashawishi vizuri, watakuwa tayari kukuchangia uanze biashara. Kama watu wanaweza kuchangia harusi na mambo mengine, wanaweza pia kuchangia biashara, ni wewe uweze kuwashawishi vizuri. Ila hapa unahitaji kuwa unaaminika na ndugu hao n apia waoneshe ni jinsi gani wao watanufaika na biashara utakayoanzisha.
  1. Kutafuta mtu au watu wa kushirikiana nao.
Kwa uzoefu wetu, kuna watu wengi ambao wana mitaji ya kibiashara ila hawajui ni biashara gani wafanye au hawana muda w akusimamia biashara. Na wakianzisha biashara kwa sababu hawana usimamizi mzuri wanapata hasara. Sasa wewe unahitaji kuwajua watu wa aina hii na andaa mpango ambao utawashirikisha na kuonesha ni kwa jinsi gani mkiungana pamoja mnaweza kuwa na biashara nzuri na yenye faida. Hii pia inahitaji uwe unaaminika na yule unayempelekea mpango wako.
  1. Kuanza biashara kwa fedha za mteja.
Hapa unaweza kukusanya fedha kwa wateja kwanza halafu ndio ukawapata huduma au bidhaa wanayohitaji. Kama utaweza kuwa na mpango mzuri wa biashara ambapo mteja anahitaji sana unachotoa, na tayari anakuamini anaweza kukupa sehemu ya gharama na wewe kutumia gharama hiyo kumpatia bidhaa au huduma anayotaka. Hii pia inahitaji uaminifu na wale unaofanya nao biashara.
Hii ndio njia ambayo inafahamika na kila mtu na watu ndio huwa wanaifikiria hii kila wanapofikiria mkopo wa biashara. Kama una sifa za kupata mkopo unaweza kuchukua mkopo na kuutumia kwenye biashara. Ila kuwa makini sana kama unachukua mkopo kwa ajili ya kuanzia biashara, ni hatari sana na unaweza kujiingiza kwenye matatizo zaidi.
Bado unafikiria ni njia gani unazoweza kutumia kupata mkopo wa biashara? Anza na hizo hapo juu na boresha kadiri biashara yako ilivyo na wale wanaokuzunguka walivyo. Hakuna kitu kinachoshindikana kama utaamua kweli kupata mkopo wa biashara.