Friday, May 27, 2016

Rekodi ya ubingwa Yanga

Kikosi-cha-yanga-machi-bongosoka

Yanga imefanikiwa kuweka rekodi ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara kwa mara ya 26 mwaka huu, ubingwa ambao tangu kuanzishwa kwa Ligi Kuu Tanzania Bara hakuna timu yoyote iliyofikia idadi hiyo.
Simba ya Dar es Salaam yenye upinzani na Yanga inashika nafasi ya pili ikiwa imetwaa mara 18. Pia  Mrundi Amissi Tambwe  amevunja rekodi kwa  kufunga mabao 21 hadi sasa katika ligi hiyo na kuvunja rekodi ya Abdallah Juma aliyefunga mabao hayo 20 ndani ya kipindi cha miaka 10 iliyopita.
Rekodi ya kufunga mabao mengi inashikiliwa na Mohammed Hussein ‘Mmachinga’ aliyefunga mabao 24 katika ligi hiyo mwaka 1994. Tambwe pia ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa kigeni nchini kufunga zaidi ya mabao 20 katika ligi Tanzania.

Tambwe pia ameweka rekodi mpya ya kuwa mchezaji mwenye mabao mengi zaidi Ligi Kuu Tanzania Bara ndani ya kipindi cha misimu mitatu tu baada ya kufunga mabao 54.

0 comments:

Post a Comment