Friday, June 3, 2016

JINSI YA KUDUMISHA MAPENZI YENU


KUWA NA MUONEKANO CHANYA  KWA MPENZI WAKO.
Ukiwa Ni Mtu Wa Kuangalia Mabaya/Kasoro Sana Kwa Mpenzi Wako Kuliko Mazuri Yake Hautakuja Kukaa Kwenye Relationship Kwa Muda Mrefu Hata Siku Moja...Utaendelea Kubadilisha Wanaume/Wanawake Kila Siku Na Mwisho Wa Siku Utajiona Huna Bahati Kwenye Mapenzi Na Wakati Unayeyaharibu Mapenzi Yako Ni Wewe Mwenyewe...Hakuna Asiye Na Kasoro (Ukiwemo Wewe Mwenyewe). Kwa Hiyo Muonyeshe Mpenzi Wako Mapenzi Bora Na Umrekebishe Pale Anapokosea Bila Kuwa Na Lawama Mara Kwa Mara, Kuna Makosa Mengine Ni Madogo Sana Na Unaweza Kuyarekebisha Kwa Kukaa Chini Na Mpenzi Wako Mkayamaliza Kwa Dakika 5 Tu Lakini Wengine Huwa Issue Kubwa Kwao Na Kusababisha Mwisho Mbaya.

TAMBUA THAMANI YAKO 
Ili uweze kuwa bora ni lazima uanzie kwako, ujitambue kama mwanamke na thamani yako kwa mwanaume wako.  Ukiijua thamani yako, lazima utakuwa makini na kila kitu. Rafiki yangu, ninaposema thamani ninamaanisha kwanza kujiamini na kujipa nafasi ya kwanza.

Uamini kwamba wewe ni mwanamke mrembo na unayevutia. Imani hiyo ikishaingia, tayari utakuwa unajali mambo mengi ya msingi, ikiwemo usafi wako binafsi. Waswahili wanasema, mwanamke ni pambo la nyumba. Pambo haina maana ya ua, inamaanisha ule usafi wa kila kitu.

Kwamba nyumba bila mwanamke haiwezi kukamilika, wewe kama mwanamke unatakiwa kufahamu wewe ni kila kitu ndani ya nyumba. Umakini wako na kujitambua ndiyo vitu vitakavyokuweka katika nafasi nzuri ya kudumu katika uhusiano wako na baadaye kuingia kwenye ndoa.

TAMBUA THAMANI YAKE
Ukiijua thamani ya mwanaume kutoka ndani ya moyo wako ni wazi kwamba hata vipengele vifuatavyo hapa chini havitakuwa vigumu kwako kutekelezeka. Inakupasa ujue thamani ya mwanaume wako ipasavyo.

Hilo si tu kwa maneno, bali ni jambo ambalo linatakiwa kufanyika kwa ridhaa ya moyo wako. Ni rahisi zaidi jambo hili kufanyika ikiwa utakuwa na mapenzi ya dhati. Mpende kwa moyo wako wote na ujue kuwa maisha yako yanakamilishwa na uwepo wake.
Ndiyo! Yanakamilishwa na uwepo wake, maana una mategemeo ya kuingia katika ndoa naye. Hapo mtakuwa mwili mmoja na maisha ya kila mmoja yatamtegemea mwenzake.


MAWASILIANO MARA KWA MARA.
Mawasiliano ni nguzo muhimu sana baina ya wapendanao, humfanya kila mtu kuhisi uwepo wa mwenzi wake hata kama atakuwa mbali naye.
Hivyo, kama una mpenzi wako aliye mbali nawe hakikisha unakuwa naye karibu kwa kumtumia ama sms, email, kadi au simu.
Aidha, pindi mnapowasiliana hakikisha humkwazi mwenzako kwa namna yoyote ile, kwani kuna watu wengi wanatabia ya kudharau baadhi ya mambo kutokana na kutingwa na shughuli kadha wa kadha, naomba nikuweke wazi kuwa hata kama umebanwa vipi pindi mpenzi wako aliye mbali anapokutumia ujumbe kwenye simu yako basi usisite kumjibu katika muda muafaka na siyo kuuchuna hadi ulalamikiwe!
HESHIMU HISIA ZAKO.
Mapenzi ya kweli yametawaliwa na hisia kali ambazo ndizo huwafanya wapendanao kufikishana kwenye mambo fulani kwani pasipo hisia hata uwe na ujuzi au utundu wakutosha hutapata raha ya mapenzi.
Kama kweli unampenda kwa dhati mwenza wako na mmetengana kutokana na sababu za kimasomo ama kazi kwa hakika utakuwa tayari kumtunzia penzi lake hadi mtakapokutana tena.
Uaminifu pekee ndio utakaokufanya uwasiliane mara kwa mara na mwenza wako na kwenye uaminifu mapenzi hushamiri huku kila mmoja akimuonea wivu wa hapa na pale mwenzi wake (lakini sio ule wakubomoa!) Hivyo heshimu hisia zako kama kweli unampenda mwenzi wako kwa kumuonesha unampenda.

SAMEHE NA KUSAHAU.
Unapomsamehe mpenzi wako kwa kosa lolote alilokosa basi hakikisha umemsamehe kiukweli na ujitahidi kusahau kosa alilotenda itasaidia uwe na amani ya moyo zaidi kuliko kumsamehe kwa usoni tu lakini moyoni ukawa na Donge bado, hii hupelekea kupunguza mapenzi kwa kiasi Fulani kwake na kujikosesha furaha ya mapenzi.Anapokosea siku nyingine usimkumbushe kosa lake la nyuma kwa sababu itamfanya ajione mwenye huzuni na ajione kuwa hakusamehewa

0 comments:

Post a Comment